September 09, 2009

KIWAKKUKI KUFUNDISHA NAMNA YA KUKABILI MSONGO MAWAZO KAZINI

Shirika la KIWAKKUKI Kilimanjaro limeanza utaratibu wa kutoa mafunzo ya Jinsi ya kukabili msongo mawazo kwa wafanyakazi wake na kwa wanaojitolea.
Akifafanua haya mkuu wa kitengo cha kukabiliana na Msongo mawazo kazni Dr. A.Mtalo alisema kuwa Msongo ni hali ambayo hutokea kwa watu binasfi, makundi, shirika n.k, hivyo KIWAKKUKI kama tunavyofahamu kuwa tunafanyakazi katika hali Ambazo zinaweza kusababisha msongo, hivyo tumeona ni vema tukapeana semina hii Ambazo mwisho wa siku washiriki watakuwa waelimishaji msingi wa Msongo mawazo kwa lengo la kuwaelimisha wengine

Dr. Mtalo aliendelea kusema kuwa wanalishukuru shirika la Antares la Uholanzi kwa kuanzisha programu hii KIWAKKUKI kwani ni programu ya muhimu na itakayoleta mabadiliko “ Tunalishukuru shirika la Antares kwa kuona kuwa kuna kila sababu ya kwa KIWAKKUKI kuwa na mafunzo haya ili kuweza kukabiliana na Msongo Mawazo ambao huweza kumpata mfanyakazi /anayejitolea au kwa yeyote ambaye anafanya shughuli za KIWAKKUKI”.

Imeonekana kuwa endapo msongo/visababishi vinavyochangia msongo mawazo endapo havitadhibitiwa mapema, inaweza kusababisha utendaji kazi kulegalega na hatimaye kushindwa kabisa kusaidia jamii kama ilivyolengo la KIWAKKUKI.

Mwaka 2004 wataalamu wa masuala ya Msongo walifika KIWAKKUKI na kuandaa dodoso linaloonesha visababishi vya msongo kutoka kwa wanaojitolea na wafanyakazi.

Baada ya kukusanya data kupitia madodoso, wataalamu hawa walirejea nchini kwao Uholanzi na mnamo mwaka 2008 aprili walifika tena KIWAKKUKI kwa lengo la kutoa mafunzo kwa wakuu wa Timu kwa lengo la kuendeleza elimu hii zaidi.
Katika mafunzo hayo yalihusisha Waratibu wa KIWAKKUKI wilayani ,Wawakilishi wa KIWAKKUKI wa wilaya na wanaojitolea toka wilaya zote sita (Same,Mwanga,Rombo,Hai,Moshi Mjinina Moshi vijijini) kwa lengo la kutoa elimu hii ili watakaoelimishwa waweze kuelimisha vikundi vingine.

Awali wataalamu hawa walikuwa wakitoa mafunzo ya kukabiliana na msongo kwa watu waliokuwa wanafanyakazi katika maeneo hatarishi mfano vitani,hospitalini n.k

Mnamo mwaka 2008 mwezi wa 11, wataalamu hawa walikuja tena kwa ajili ya kufuatilia na kuwawezesha wakufunzi kuwa na uwezo wa kwenda kufundisha wengine

Elimu hiyo hutolewa kwa kuangalia Mambo yanayochangia msongo Mawazo, dalili za msongo mawazo,athari za msongo mawazo,na Namna ya kukabiliana na Msongo mawazo

Kwa upande wa wafanyakazi walioko ofisi kuu hupata fursa kufanya mazoezi mbalimbali yanyosaidia kukabiliana na msongo mawazo.Mazoezi hayo yanahusu zaidi suala la kuchua sehemu mbalimbali za mwili na kuruhusu msongo utoweke mwilini.Sehemu hizo ni pamoja na uso, pua, vidole, shingo, miguu, mdomo wa juu na chini, masikio n.k

Picha na matukio mbalimbali:

Mweka hazina wa KIWAKKUKI J.Kanza akifungua rasmi semina ya kukabiliana na Msongo mawazo tarehe 28 april 2009


Theresia Sabuni (Aliyesimama mbele)mmoja wa wakufunzi na msimamizi wa mafunzo KIWAKKUKI akifundisha moja ya mada ya kukabili msongo mawazo(Picha juu)


Msimamizi wa kitengo cha kukabili msongo mawazo(Dr. Mtalo) akiongoza washiriki katika zoezi la kusua misuli ili kuondoa msongo


Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kukabiliana na msongo mawazo wakijadiliana katika moja ya kazi ya vikundi


Romana Mallya mmoja wa washiriki wa mafunzo akiwasilisha kazi ilifanywa na kikundi kuhusu namna ya kukabili msongo mawazo

1 comment:

Anonymous said...

Trish
You have no idea how much I have enjoyed reading this post! It makes me want to buy a plane ticket and rush right to KIWAKKUKI. I miss all of my mamas very much. But mostly, I miss doing work with such purpose, surrounded by amazing people.
Thank you for keeping me up to date on all things KIWAKKUKI.

-Jen Lajoie