September 08, 2009

UTAFITI KUHUSU MATOKEO MAZURI YA WATOTO YATIMA KIWAKKUKI

Ni Utafiti wa ufuatiliaji unaofanyika katika nchi mbalimbali unaotafuta kutambua viashiria vya matokeo mazuri kwa Watoto yatima.

Hapa Tanzania Utafiti huu unafanyika katika mikoa ya Kiliamanjaro na Arusha. Katika mkoa wa Kilimanjaro ni wilaya za Moshi vijijini, Manispaa, Hai na Siha. Katika mkoa wa Arusha ni wilaya ya Arumeru.

Madhumuni:
Kupata uelewa ili kuweza kushauri/ kushawishi wadau mbalimbali( kwa mfano Watunga sera, Mashirika ya fedha na walezi) kuhusu mila na desturi za malezi ambazo zinahitaji kuzingatiwa wakati wa mipango ya kusaidia watoto yatima.

Lengo kuu:
Kutumia matokeo ya utafiti huu kuboresha malezi ya watoto yatima kwa kupitia mipango itakayowekwa hapa na kwingine duniani.

KWANINI UTAFITI HUU UNAFANYIKA:
1. Kuna haja kutatua matatizo- Je tunajua ni katika mazingira gani mtoto anapata malezi bora zaidi ni kwenye Jamii au Vituo- Ni nini kinatuonyesha kwanini Watoto wengine wanafanya vizuri zaidi na wengine wanashindwa.- Ni wapi pengine tuwekeze fedha za malezi ya Watoto Yatima- Je tumeisha yaorodhesha matatizo au sababu za matatizo ya Watoto yatima.
2. Itatupatia mwanga au majibu ya muundo na mahusiano kwenya jamii

NJIA ZILIZOTUMIKA KUFUATILIA
Watoto wote hawa wanafuatiliwa kila baada ya miezi sita kwa kipindi cha miaka mitatu. Wanafuatiliwa na kufanyiwa usaili unaotaka kujua hali za Afya za watoto, Elimu ya mtoto, Chakula, malazi, Msongo wa mawazo na Hali ya kipato cha familia. Washiriki wakuu katika ufuatiliaji huu ni(rasilimali watu):Watendaji wa kata, Wenyeviti wa mitaa, Wenyeviti wa vijiji, Wasaili, Walezi, Watoto na Walimu. Njia kuu tunazotumia kukusanya taarifa ni mahojiano ya moja kwa moja.

WASHIRIKI NA MAENEO YA KUSHIRIKI

Washiriki na maeneo wanayotoka walichaguliwa kwa kutumia mfumo maalumu wa namba kuwachagua ili kuepuka upendeleo.

KWA MAELEZO ZAIDI :TEMBELEA OFISI ZA TAWREF BARABARA YA NYERERE MKABALA NA SOKO KUU LA MOSHI

No comments: