September 08, 2009

WANAFUNZI WA JITEGEMEE PASUA WANG'ARA


Shirika lisilo la kiserikali la Wanawake Kilimanjaro limetoa misaada mbali mbali kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa Kilimanjaro
Katika hatua zake za kusaidia serikali kukabiliana na ongezeko la watoto Yatima, KIWAKKUKI imeweza kuwasaidia watoto 6 wa shule ya Msingi Jitegemee Moshi ndani ya Kata ya Pasua kwa kuwapatia sare za shule, madaftari pamoja na kuwalipia michango ya chakula ili waweze kukaa darasani na kusikiliza wanachofundishwa.
Hawa ni wachache kati ya wengi ambao wamenufaika kupitia mradi huo wa watoto Yatima.
Watoto hawa walipata msaada huo kutoka kwa baadhi ya familia zenye mapenzi mema na jamii ya tanzania toka Marekani ambao ni familia ya Dorean Weiss.
Hatua ya familia hii kuanza kusaidia zilitokana na jitihada za mtoto wao aliyekuwa akijitolea KIWAKKUKI mwaka 2007.


No comments: