Hali hii imedhihirika baada ya wafanyakazi hao kuiona kuna umuhimu wa kukaa pamoja na kuwaanga ama kuwapongeza wenzao
Mwenyekiti wa KIWAKKUKI mama Imaculate Mrema alihudhuria hafla hiyo iliyokuwa imeandaliwa na wafanyakazi wanaoendelea na mikataba yao ya ajira.
“Hatua hii ni nzuri maana inapunguza msongo mawazo na kuleta burudani miongoni mwa wafanyakazi” alisema mmoja wa wafanyakazi ambaye alionekana muda wote kuwa mwenyefuraha isiyo kifani.
Hafla hii iliambatana na chakula pamoja na viburudisho kemkemi ndani ya ukumbi mpya wa KIWAKKUKI katika kata ya Korongoni Mjini Moshi.Kadhalika kulikuwa na ma “DJ” ambao walionesha umahiri wao wa kurusha muziki kwa mpangilio uliovutia wengi. “He! Hii kali, huwezi kuamini tunao ma Dj na ma MC humu hakuna sababu ya kukodisha tena MC” alisikika mmoja wa wafanyakazi ambaye alikuwa muda wote akitikisa kichwa chake kwa ladha ya muziki ulivyokuwa ukirindima.
Kadhalika wafanyakazi waagwa walipata fursa ya kuzungumza ambapo zaidi walisema wanashukuru kwa zoezi hili la kuwaaga kwani limeonesha kuwa upendo miongoni mwa wafanyakazi wa KIWAKKUKI .Hivyo waliomba upendo huu udumu na uendelee hata kwa wengine
Wafanyakazi walioagwa ni:
H.G. Ndanu-Fundi sanifu maabara
Mama Shangali-Mshauri Nasihi
Rehema Kiwera-(Aliwakilishwa na Petronila) Mkuu wa Idara ya Kutembelea wagonjwa nyumbani
Joyce Kinabo-Mtembeleaji wagonjwa Nyumbani(Aliwakilishwa na S.B.Moshi)
Piala Arkard -Mtembeleaji wagonjwa Nyumbani
A.Mgonjna- Mkuu wa kitengo cha ushauri nasihi(Aliwakilishwa na A.Mwalla)
Salvatory A.Chami- Dereva
Picha na Matukio
Baadhi ya wafanyakazi waagwa wakipokea zawadi za pongezi toka kwa mwenyekiti wa KIWAKKUKI I.Mrema
Sehemu ya wafanyakazi wa KIWAKKUKI wakicheza “Twist” pamoja na mwenyekiti kuonesha furaha waliyonayo huku wengine wakiwashangilia
No comments:
Post a Comment